BANDA AIKOMBA SIMBA MILIONI 65

Mchezaji wa timu ya soka ya Simba Abdi Banda amethibitisha kukaa na viongozi wa timu hiyo na kujadili juu ya kuongeza mkataba mpya baada ya ule wa awali kusalia siku tano kuweza kumalizika.


Banda ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kuwa yeye na manager wake Abdul Bozinia wameshafanya mazungumzo ya awali na kila kitu kimekaa sawa kwa ajili ya kuongeza kandarasi mpya.


"Mimi mkataba wangu zimebaki siku tano umalizike lakini naweza nikaendelea nao (Simba) na naweza kusaini ndani ya siku hizi au nikirudi kutoka Afrika kusini kwenye timu ya taifa"alisema Banda.


Banda alisema kwamba aliishazunguza  na uongozi wa wekundu hao kuwa Dau lake anataka milioni 65 na washaelewana hadi juu ya mshahara wake.

"Dau langu wenyewe wanajua na nishawaambia kuwa nataka milioni 65 na tulishaelewana kila kitu hadi mshahara  na kwa sasa kinachochelewesha ni swala la meneja wangu ambae yuko safarini lakini wakati wowote kuanzia sasa atarudi na mimi nitakamilisha hilo la kusaini"aliongeza Banda.

Banda anatarajia kuondoka juni 22 mwaka huu na timu ya Taifa kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya COSAFA na akirudi huwenda mambo yote yakawa sawa na kuendelea kuichezea klabu ya simba.

Awali mchezaji huyo alikataa kusaini kandarasi mpya ndani ya klabu ya Simba akidiriki kusema kuwa malengo yake yalikuwa kwenda kucheza soka la kulipwa.

No comments