HARUNA NIYONZIMA ASEMA HAYA KUHUSU YEYE KUJIUNGA NA SIMBA

Kiungo tegemeo wa timu ya soka ya Yanga,Haruna Niyonzima amesema kwamba yeye bado hajasaini mkataba na klabu yeyote kwa ajili ya kuitumikia katika msimu ujao wa ligi.

Niyonzima aliambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kwa sasa hapendi kuzungumzia maswala ya usajili kwa kuwa yupo likizo na bado mkataba wake na klabu ya Yanga haujamalizika hivyo kwa kipindi hiki asingependa kuzungumzia jambo hilo.

Aidha alisema kwamba yeye ni mfanya biashara anaweza kuzungumza na mtu yeyote lakini kwa sasa hana nafasi ya kuweka bayana maswala yake ya usajili.

Alisema kwamba wakati utakapofika wadau watafahamu wapi ataelekea lkn kwa kipindi hiki ni vyema wakamuacha ashughulikie maswala yake ya kifamilia.

No comments