FRIENDS RENGERS WAUKATAA UWANJA WA LIPULI

Uongozi wa timu ya soka ya Friends Rengers ya jijini Dar es salaam,umesema kwamba kikosi chao kimejiandaa vyema kuwakabili Ashaniti hapo kesho katika mchezo wa ligi daraja la kwanza unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Karume.

Meneja wa timu hiyo,Shabani Masilah,amesema kwamba kwa upande wao kama viongozi wamejipanga vyema kwa ajili ya mchezo huo kwani pointi tatu kwenye pambano hilo zitakuiwa na tija kwao hasa katika harakati za kufanikiwa kupanda ligi kuu ya Tanzania.

Masilah amesema kwamba,mbali na mchezo huo pia wamelitaarifu shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,kuhusiana mchezo wao dhidi ya Lipuli unaotaraji kupigwa tarehe 28 mkoani Iringa.

Amesema kwamba kwa upande wao wametoa taarifa za kukosa Imani na uwanja unaotumiwa na wenyeji wao Lipuli,kwani kumetokea vuruga katika mechi mbaili zilizochezwa kwenye uwanja huo na kusababisha baadhi ya wachezaji na mashabiki kujeruhiwa na mashabiki wanaosadikiwa na wa Lipuli.

No comments