YANGA WAUKATAA MCHEZO WAO DHIDI YA MAJIMAJI

Wakati ratiba ya ligi kuu ya Tanzania bara ikionyesha kuwa siku ya jumanne ya tarehe 17 ya mwezi huu kunataraji kuchezwa mchezo kati ya Majimaji na Yanga kwenye uwanja wa Majimaji,kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kwamba hafahamu ratiba ya mchezo huo na kwa sasa kikosi cha timu hiyo bado kipo Dar es salaam.

Mwambusi ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kama yeye ni miongoni mwa viongozi wa benchi la ufundi hafahamu mchezo huo kuchezwa siku ya jumanne bali kilichopo ni kuwauliza viongozi wa klabu ili kufahamu ratiba kamili ya mechi hiyo itakayochezwa Songea mkoani Ruvuma.

Yanga iliwapa mapumziko ya siku mbili wachezaji wa timu hiyo baada ya kurejea kutoka Zanzibar,kufuatia kushindwa kutinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi kwa kufungwa na watani wao wa jadi Simba kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-2.

No comments