POLISI WAIMARISHA ULINZI KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA

Kamanda wa Polisi wa mkoa mjini Magharibi Unguja,Hassan Nasri amesema kwamba kwa upande wao wamejipanga vyema kuwahakikisha hali ya usalama inakuwa bora kuelekea kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga,mechi inayotaraji kupigwa kuanza mishale ya saa mbili usiku.

Nasri amewataka mashabiki ambao wana nia ya kufanya vurugu,kusitisha mara moja mpango huo kwani kwa upande wao wamejipanga kikamilifu kuhakikisha mechi hiyo inachezwa pasipo vurugu zozote.

Amesema kwamba ni vyema mashabiki wakakata tiketi zao mapema ili kuondoa usumbufu utakaojitokeza uwanjani hapo.

No comments