MAJIMAJI KUUMANA NA YANGA HAPO KESHO

Ligi kuu ya Tanzania bara inataraji kuendelea kesho kwa mchezo mmoja,ambapo wanalizombe wa Songea timu ya Majimaji itakuwa nyumbani kuwakaribisha mabingwa watetezi wa kombe hilo Young Africans.

Kuelekea kwenye mchezo huo,shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba kwa upande wao maandalizi yamekamilika katika pambano hilo na wanataraji kuona idadi ya mashabiki ikiwa kubwa kwenye mtanange huo,hii inatokana na kasumba ya mashabiki wa mkoani Ruvuma kujitokeza kwa wingi kushuhudia timu yao inapocheza.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mbali na mchezo huo,pia ligi hiyo itaendelea tena kwa siku ya jumatano kwa michezo miwili kuchezwa katika viwanja tofauti.

Mkoani Morogoro Mtibwa Sugar itawakaribisha wekundu wa msimbazi timu ya soka ya Simba,mechi itayochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri kuanzia mishale ya saa kumi huku Azam FC itakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani kumenyana na wagonga nyundo wa mkoani Mbeya,timu ya Mbeya City.

No comments