HAKUNA MABADILIKO JUU YA MECHI YA MAJIMAJI NA YANGA

Uongozi wa bodi ya ligi ambao ndio wasimamizi wa ligi kuu ya Tanzania bara,umesema kwamba mechi ya Majimaji na Yanga itachezwa siku ya jumanne kama ilivyopangwa na hakuna marekebisho yeyeote ambayo wameyafanya juu ya mchezo huo.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi,Boniphace Wambura ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba klabu zote zimeshafahamishwa juu ya ratiba ya michezo hiyo hivyo hawatarajii kuona klabu inalalamika kutofahamu tarehe ya michezo yao.

Wambura amesema kwamba Bodi ya ligi imefanya marekebisho kwa baadhi ya mechi ambazo hazikupangiwa tarehe kwa ajili ya kupisha michuano ya kombe la mapinduzi kwa timu za Yanga,Simba pamoja na Azam lakini kwa sasa mechi hizo tayari zishapangiwa tarehe na kila timu imeshafahamishwa.

No comments