MPIRA PESA WAWAPONGEZA WAAMUZI WA ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Tawi la Simba la Mpira Pesa,Hustadhi Masoud amesema kwamba kwa upande wao kama mashabiki wa timu hiyo wana matumaini makubwa ya timu yao kuibuka na ushindi mbele ya Yanga hapoa kesho.

Masoud amesema kwamba Yanga ni timu ya kawaida na mara nyingi imekuwa ikipata matokeo mazuri kwao kwa sababu waamuzi wamekuwa wakishindwa kufuata sharia 17 za soka.

Amesema kuelekea kwenye mechi ya kesho Simba ina nafasi kubwa ya kushinda kwa waamuzi wa Zanzibar wamenyesha uweelewa mzuri wa kutafasiri sharia 17 za mpira wa miguu.

No comments