BODI YA LIGI YAPANGUA RATIBA FDL

Mechi za raundi ya 11 katika makundi yote ya ABC za ligi daraja la kwanza ambazo zilipangwa kuchezwa kati ya januari 13 na 14 mwaka huu zimeondolewa, na sasa zitafanyika kati ya februari 17 na 19.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi,Boniphace Wambura amesema kwamba sababu za mabadiliko hayo ni kupisha mechi zote za raundi ya nne ya michuano ya kombe la Azam sports Federation itakayoshirikisha timu za daraja la kwanza FDL ambapo zitachezwa januari 14 na 16.

No comments