AZAM WAWAPA ZAWADI YA KOMBE MASHABIKI WAO

Uongozi wa Azam FC,umesema kwamba kwa upande wao kama viongozi wa klabu hiyo kwa dhamira kubwa wanawapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kufanikisha kuwa mabingwa wa kombe la mapinduzi kwa mara ya tatu.

Afisa Habari wa Azam,Jafary Idd amesema kwamba kama wao viongozi wamefurahishwa na ushindi huo kwani si kazi rahisi kwa wao kufanikiwa kuwa mabingwa.

Jafary Idd amesema kwamba ushindi huo moja kwa moja wanatoa zawadi kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kuendelea kuinga mkono timu hiyo yenye makazi yaka Chamazi,nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Aidha amesema kwamba kikosi leo hii kinarejea kikitokea Zanzibar na wachezaji watapewa mapumziko kwa siku yah ii kabla ya kurejea tena kambini hapo kesho kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Mbeya City.

No comments