RAGE AWAPONGEZA WAAMUZI WA ZANZIBAR

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba,Ismail Aden Rage amewapongeza waamuzi wa Zanzibar kwa kufanikiwa kutafasiri vyema sharia 17 katika mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga ikiwa ni mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kombe la mapinduzi.

Rage amesema kwamba kwenye mechi hiyo waamuzi wamelitendea haki pambano hilo ambalo mara nyingi huwa waamuzi huwa wanashindwa kulimudu vizuri.

Amesema kwamba mwamuzi wa kati amepata msada mkubwa kutoka kwa wasaidizi wake na kasoro zilizokuwepo ni chache ambazo zikifanyiwa kazi zitawafanya kuwa bora Zaidi.

No comments