KAULI YA MAYANJA BAADA YA KUWAFUNGA YANGA

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Simba,Jackson Mayanja amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kupambana kuhakikisha wanatinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya kombe la mapinduzi.

Mayanja ameyasema hayo kufuatia Simba kuibuka na ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-2 mbele ya Yanga baada ya dakika 90 timu hizo kushindwa kufungana.

Amesema kwamba mipango yao ilikuwa ni kuingia fainali hivyo matokeo hayo ambayo wameyapata ni mazuri kwao na kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam Fc.

No comments