STEND UNITED WAWEKA BAYANA SIRI YA MAFANIKIO YAO YA KUANZA VYEMA
Uongozi wa klabu ya Stend United ya mkoani Shinyanga umesema kwamba kufanya kwao vizuri tangu kuanza kwa msimu ni kuwa na maandalizi mazuri kabla ya ligi pamoja na viongozi wa klabu hiyo kuwajenga kisaikolijia wachezaji wa timu hiyo.
Msemaji wa timu hiyo Deo Kaji Makomba
 ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kulikuwa na maneno mengi kutoka kwa baadhi ya wadau wa 
soka wakidiriki kusema timu hiyo ingeshuka daraja hasa baada ya kuwepo 
na mgogoro uliyowahusisha viongozi wa Kampuni na wanachama lakini kwa kutambua umuhimu 
wa timu hiyo wamejizatiti kuiongoza vyema.
Aidha katika hatua nyingine Makomba amesema
 kwamba swala la uendeshaji timu limekuwa tatizo kutokana na fedha 
zinazotelewa na wadhamini wa ligi hiyo kutokizi matakwa yao ya 
uendeshaji lakini kama wao viongozi wanaendelea kupigana kuondokana na 
adha hiyo ya ukata.
Hata
 hivyo Makomba amekili kuwa kwa sasa uongozi wa klabu hiyo upo katika 
mazunguzmo na kampuni ya ACACIA kuona ni jinisi gani wanamaliza tatizo 
lililopo hasa baada ya kampuni hiyo kutangaza kujiondoa kuidhamini timu 
hiyo baada ya kuwepo na mgogoro hapo awali.
"Sisis bado tunatambuwa kuwa mdhamini wetu bado ni ACACIA hivyo kama kuna upande unataka kuvunja mkataba basi ni vyema ukafuata taratibu ikiwemo kutoa notisi na pia kuwepo na maeleano ya uvunjaji wa mkataba huo lakini naamini hilo swala litakwisha kwani tumeshaanza mchakato wa kulitatua tatizo hilo"alisema Makomba. 

Post a Comment