KISA AGIZO LA MAHAKAMA MANJI AFUTA MKUTANO MKUU WA ZARURA
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yussuf Manji ameridhia agizo la mahakama kwa kuamua kuufuta mkutano mkuu wa zarura ambao ulitarajiwa kufanyika siku ya kesho katika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Manji amesema kwamba siku ya jana alipokea barua kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikitoa katazo la kutofanya mkutano huo kufuatia baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kufungua kesi ya kupinga mkutano huo.
Manji amesema kwamba ingawa hatua hiyo imeleta athari kwa upande wao lakini hana budi kuufuta mkutano huo kwani Yanga imeundwa kwa misingi ya kufuata katiba ya nchi.
Katika hatua nyingine Manji amesema kwamba kwa sasa hawezi kuongelea sana juu ya zuio hilo kwa kuwa kitu ambacho kipo mahakamani hakipaswi kuzunguzwa pasipo taratibu kamili.
Hata hivyo amesema kwamba pia wanachama hao ambao wameenda mahakamani wanapaswa kufahamu kuwa katiba ya Yanga inasema kuwa kwa yule mwanacha atakaenda mahakamani kuhusiana na maswala ya klabu basi moja kwa moja amejifuta uwanachama.
Post a Comment