WANASHERIA VIJANA WAMJIA JUU YUSUPHU MANJI KATIKA SWALA LA UKODISHWAJI WA TIMU

Wanasheria vijana ambao ni wanachama wa klabu ya Yanga kwa kauli moja wamepingana na maamuzi ya ukodishwaji wa klabu ya Yanga wakidai kuwa taratibu ambazo zimefanyika ni batili.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii aliyewai kuwa mwanasheria wa klabu hiyo Frenk Chacha amesema kwamba anashangaa kuona klabu ya Yanga inakodishwa na watu ambao hawana mamlaka ya kufanya hivyo kwani hawastahili.

Chacha amesema kwamba baraza la wadhamini ambao wamechukuwa jukumu la kuikodisha timu muda wao ulishaisha na pia wengi wao hawamo katika baraza hilo.

Amesema kwamba kutokana na jambo hilo kama wao wanasheria vijana wa Yanga hawakubaliani na maamuzi ya ukodishwaji wa miaka 10 kwa klabu ya Yanga kwani viongozi husika wakiongozwa na mwenyekiti Yusuph Manji wamekiuka maadili na katiba ya Yanga.

No comments