WAZEE WA YANGA WASEMA YANGA HAIKODISHWI KAMA MASUFURIA

Katibu wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga Ibrahimu Akilimali amesema kwamba kwa upande wao kama wazee na wanachama wa klabu hiyo hawakubaliani na maamuzi yaliyofanywa na baraza la wadhamini wa klabu hiyo kuchukua jukumu la kukodisha timu kwa kampuni iliyopewa jina la Yanga yetu kwa kipindi cha miaka 10.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Akilimali amesema kwamba kwa upande wao hawautambui ukodishwaji huo kwani taratibu ambazo zimetumika hazikizi matakwa ya katiba ya klabu ya Yanga.

Amesema kwamba mwenyekiti wa klabu hiyo kwanza ameisgina katiba hasa mara baada ya kuitisha mkutano usio halali na kujipangia mamlaka ya kutaka kuikodisha timu pasipo akidi ya wajumbe husika kukubaliana.

"Mkutano unaitishwa bila ya wajumbe kukubaliana alafu mnafika kwenye mkutano mtu mmoja anajipangia ajenda za kuzungumza alafu  hapohapo unawafuta wanacha bila ya misingi yeyote ya katiba ya klabu,hii sio sheria ya katiba ya Yanga"alisema Akilimali.

Aidha amedai kuwa kwa kitendo hiki ambacho anakifanya mwenyekiti wa Yanga juu ya ukodishwaji wa timu anaamini kutaibuka mgogoro wa Zamani ambao ulihusisha Yanga Asili na Yanga Kampuni kwa kuwa wao hawatakubaliana na jambo hilo.

No comments