TFF YASIKITISHWA NA VURUGU ZA MASHABIKI WA COASTAL UNION

Baada ya mashabiki wa Coastal Union kuchukua jukumu la kumshambulia mwamuzi Thomas Mkombozi kutoka mkoani Arusha kwa madai ya mwamuzi huyo kushindwa kutafasiri vizuri sheria 17,Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limelaani vikali tukio hilo ambalo si la kiungwana katika sekta ya michezo.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kabla ya kupokea taarifa kutoka kwa wahusika wa mchezo huo lakini shirikisho hilo linalaani vikali kwani kwa mashabiki wa Coastal Union hii siyo mara ya kwanza kufanya jambo hilo.


Lucas amesema kwamba kwa sasa wanasubiri lipoti kutoka kwa mwamuzi na kamishina wa mchezo pamoja na lipoti kutoka chama cha michezo mkoa wa Tanga ndani ya siku tatu ili kamati ya masaa 72 iweze kuchukua maamuzi yake kwa kile ambacho kimetokea huko mkoani Tanga baada ya mechi kuisha kwa KMC kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na kutawaliwa na vurugu kubwa.

"Nadhani mashabiki wa Coastal Union wanapaswa kubadilika kwani hii ni mara ya pili unakumbuka walishafanya vurugu kama hizi katika pambano dhidi ya Yanga ambapo mwamuzi alipigwa na jiwe,sasa haya mambo tukiyavumilia mwishoni yatakuja kuleta athari kubwa"alisema Lucas.

No comments