RECREATIVO DO LIBOLO INA WAKATI MGUMU WA KUTETEA UBINGWA WAKE

Ligi kuu ya nchini Angola maarufu kama Gira Bora inazidi kuvuta kasi wakati ligi hiyo ikielekea ukingoni huku hadi sasa timu ya Premeda Agosto na Petro Atretico de Luanda zikiwa na nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo baada kufanya vizuri katika michezo yao ya mwisho mwa juma.

Premeda Agosto ndio inaongoza ligi kwa sasa ikijikusanyia alama 60 mara baada ya kushuka dimbani katika michezo 27 huku wakifuatiwa kwa ukaribu na wapinzani wao Atretico de Luanda wenye alama 57 kwa kucheza michezo 27.

Mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Recreativo do Libolo baada ya jana kukubali kupokea kichapo cha bao 1-0 wakiwa ugenini mbele ya Proggresso wanaendelea kukaa kwenye nafasi ya tatu wakiwa na alama 54 baada ya kushuka dimbani mara 27.

Kwa mujibu wa mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga,Said Maulidi anayefundisha soka nchini humo amesema kwamba ligi ya msimu huu imekuwa na ushindani mkubwa kwani hadi sasa zikiwa zimesalia mechi tatu ligi kuisha lakini bado mshindi wa kombe hilo hajulikani.

Timu za Academica do Lobito wenye alama 25 na de Maio ambao wana alama 21 sawa na Porcelana wapo katika wakati mgumu wa kuepukana na janga la kushuka daraja kwani ndizo timu zilizo kwenye nafasi ya mwisho ya msimamo wa ligi hiyo inayohusisha jumla ya timu 16.

No comments