LICHA YA KUSHINDWA KUWAFUNGA AZAM FC,MWAMBUSI AWAPONGEZA WACHEZAJI WAKE

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga Juma Mwambusi amesema kwamba licha ya kikosi chake kushindwa kuchomoza na ushindi mbele ya Azam FC lakini vijana wake wamecheza vizuri.

Mwambusi amesema kwamba sababu kubwa ambayo imewafanya washindwe kuibuka na ushindi ni kutotumia nafasi ambazo walizipata katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na timu hizo kugawana pointi mojamoja baada ya sale ya kutofungana.
Amesema kwamba kwa sasa wanajipanga na michezo iliyo mbele yao ili waendelee kutetea taji la ubingwa wa ligi kuu kwa mara nyingine.

No comments