MANJI AWAHIMIZA WANACHAMA WA KLABU YA YANGA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MKUTANO MKUU

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Yusuphu Manji amewataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkuu wa zarura unaotaraji kufanyika siku ya jumapili katika uwanja wa mazoezi uliopo klabuni hapo.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari leo hii Manji amesema kwamba wanachama wanapaswa kufahamu kuwa mkutano huo unatija kwa upande wao kwani utawafanya wanachama hao kutoa hoja zao ambazo zitapaswa kujadiliwa na wanachama kwa ujumla.

Amesema kwamba maandalizi kuelekea kwenye mkutano huo yamekamilika ambapo usalama wa kwa kila mwanachama utakuwa ni wa kutosha hivyo ni vyema wakajitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuamua maendeleo ya klabu.

Katika hatua nyingine Manji amewataka wanachama wa klabu hiyo kuacha kuogopa vikao ambavyo vinaitishwa na uongozi wa klabu hiyo kwani kuhudhuria kwao kuna wapa nafasi ya wao kuchangia kile wakionacho.

Manji amesema kwamba anashangaa kuona baadhi ya wanachama wa klabu hiyo wanakimbilia kuzungumza kwenye vyombo vya habari huku wanashindwa kufika kwenye mikutano ya klabu.

Amesema kwamba kuelekea kwenye mkutano huo ni vyema wanachama wakajitokeza na kwa wale ambao hawajalipia kadi zao ni vyema wakazilipia mapema ili kupata fursa ya kuwepo kwani endapo usipolipia kadi hiyo itakulazimu kutokuwa mwanachama halali na hutopaswa kuwepo kwenye mkutano huo.

Hata hivyo amesema kwamba kama yeye mwenyekiti wa klabu hiyo hana mpango wa kufukuza wanachama wa klabu hiyo bali yeye anasimamia misingi na katiba ya klabu.

No comments