TFF WAENDELEA KUTOA UFAFANUZI SWALA LA HASSANI KESSY

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limeendelea kutoa ufafanuzi juu ya swala la mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kuhusiana na madai ya klabu ya Simba ya mchezaji huyo kuvunja mkataba.

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mchezaji huyo yuko huru kucheza mechi za ligi kuu ya Tanzania bara kwa kuwa kamati ya hadhi ya wachezaji ilimuidhinisha kuichezaea klabu ya Yanga kwa sasa babu viongozi wa Simba hawakuwasilisha kesi inayohusiana na maswala ya usajili.

Lucas amesema kwamba klabu ya Simba imewasilisha kesi ya madai hivyo ni jukumu la pande hizo ziweze kukubaliana jinisi namna gani wanavyoweza kulimaliza swala hilo.

No comments