AKILIMALI ASEMA AMESHAJUA MBINU ZA MANJI APANGA KUZUNGUMZA NA WANAHABARI

Katibu wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga Ibrahimu Akilimali amesema kwamba anaamini mkutano mkuu wa dharura uliotishwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji unaotaraji kufanyika siku ya tarehe 23 ya mwezi huu una ajenda za kumjadili yeye ikiwemo swala zima la kumfuta uwanacha.

Akilimali amesema kwamba mkutano huo ni mzuri kwa kuwa una mpango wa kumjadili yeye baada ya kuonekana anazungumza mara kwa mara kwenye vyombo vya habari lakini kwa upande wake juu ya jambo hilo atalitolea ufafanuzi siku ya jumatano mbele ya waandishi wa Habari katika ukombe wa idara ya Habari Maelezo.

Amesema kwamba mwanachama ana haki ya kuongea na vyombo vya Habari lakini anashangaa kuona uongozi wa klabu ya Yanga chini ya mwenyekiti wao Yusuph Manji  umekuwa ukiwafuta uanachama wale ambao wamekuwa wakifanya hivyo.

"Yani wazungumzaji wa radio mara nyingi si mzee Akilimali,Mohamed Musumi si ndio tunaozungumza kwamba hilo tunapotoa maoni yetu ni kosa kwa mujibu wa katiba ya sasa,sasa ndio tunaka tufukuzwe siku hiyo kwa hiyo sio mkutano mbaya"Akilimali alisema.

No comments