SIMBA KUWAFUATA MBEYA CITY HAPO KESHO

Kikosi cha timu ya Simba hapo kesho kinataraji kuanza safari ya kuelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao dhidi ya Mbeya City mchezo unaotaraji kuchezwa siku ya jumatano.

Meneja wa timu hiyo Musa Hassan Mgosi amesema kwamba  kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi pia hakuna mchezaji aliye  majeruhi hivyo inawapa fursa ya kwenda kufanya vyema kwenye mchezo huo unaotaraji kuwa na upinzani mkali.

Mgosi amesema kwamba baada ya kukamilika kwa mchezo wao dhidi ya Yanga ambapo timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 kwa sasa mipango yao wameielekeza katika mchezo huo dhidi ya Mbeya City ili wafanikiwe kupata alama tatu ambazo zitawafanya wakae kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Aidha Mgosi amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa sasa kuachana na habari za mchezo uliopita kwani kuendelea kuendelea kuzungumzia mchezo huo ni sawa na kupoteza muda.

No comments