HANS DAR PUIJM ASEMA WACHEZAJI WAKE WANGEKUA MAKINI MO BEJAIA ANGEFUNGWA NYINGI


Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Hans der Puijm amesema kwamba wachezaji wake wangekua makini wangeweza kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao mengi zaidi katika mchezo wa hii leo dhidi ya Mo Bejaia ambapo mabingwa hao wa ligi kuu wamefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1-0

Pluijm amesema wachezaji wake hasa wa safu ya ushambuliaji wamekosa nafasi nyingi za wazi ambapo kama wangekua makini wangeibuka na ushindi mkubwa zaidi tofauti na bao moja ambalo wamelipata

Aidha amesema kwamba licha ya kikosi cha timu hiyo kuendelea  kuwa kwenye nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi A lkn hawatakata tamaa kwani kwenye mpira lolote linaweza kutokea

Ushindi huu wa Yanga ni wa kwanza katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho katika hatua ya makundi kwani kabla ya matokeo haya ilipata sale moja kwenye mchezo dhidi ya Medeama ya nchini Ghana.

No comments