KIFUKWE ASEMA HAWATAKURUPUKA KUINGIA MKATABA NA MANJI


Mjumbe wa baraza la wadhamini la klabu ya Yanga,Francis Kifukwe amesema kwamba kwa sasa wanasubiri lipoti kutoka kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji juu ya mpango wake wa kutaka kuikodisha timu kwa miaka kumi

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,Kifukwe amesema mara baada ya kupata lipoti  ndipo watakaa na kuijadili taarifa hiyo kwa kupitia vipengele mbalimbali kabla ya kuingia mkataba

Amesema kwamba licha ya wanachama wa klabu hiyo kwa pamoja kuridhia kumkodishia timu Manji kwa miaka kumi ili yeye aweze kupewa nembo ya klabu pamoja na timu, huku ndani yake kukiwa na kipengele cha kuchukua asilimia 75 ya faida huku klabu ikipata asilimia 25 amesema jambo hilo halitakua hivyo kwani kutakua na marekebisho makubwa juu ya hayo ambayo ameyazungumza

Hata hivyo Kifukwe amewataka wanachama wa klabu ya Yanga kwa sasa kua na subra juu ya jambo hilo kwani kwa upande wao wapo makini na hawatakurupuka kuingia mkataba pasipo na maelewano mazuri kwa faida ya wanayanga.

No comments