BAADA YA YANGA NA COASTALUNION KUSHINDWA KUKAMILISHA USAJILI NAZO TIMU SABA USAJILI WAO WAONEKANA KUWA NA MAPUNGUFU
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba mbali na klabu za Yanga na Coastal Union kushindwa kuwasilisha majina ya wachezaji ambao wamewasajili msimu huu pia kuna vilabu saba vya madaraja mbalimbali ya ligi hapa nchini usajili wao umeonekana kuwepo na kasoro
Katibu mkuu wa TFF,Mwesigwa Selestine amesema kwamba vilabu
hivyo vimefanikiwa kuwasilisha usajili wao lakini kilichotokea kwamba kuna
baadhi ya taratibu hazijafuatwa
Amesema kwamba baadhi ya vilabu hivyo ni pamoja na Kiluvya
United,Frends Rengers,Africa Lyon,Mashuja,Abajalo,Mvuvuma pamoja na Kitayosa,ambapo
klabu hizo zimeshindwa kukamilisha utaratibu wa usajili kupitia mfumo wa TMS.
Hata hivyo amevitaka vilabu hivyo pamoja na klabu za Yanga
na Coastal Union ambazo kwa upande wao zimeshindwa kabisa kuwasilisha majina ya
usajili kupeleka utetezi wao mapema juu ya sababu ambazo zimewafanya kushindwa
kukamilisha jambo hilo.
Post a Comment