TFF WAIPONGEZA SIMBA KWA KUTIMIZA MIAKA 80


Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limeipongeza klabu ya Simba baada ya kutimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake katika mfumo wa soka hapa nchini

Katibu mkuu wa shirikisho hilo,Selestine Mwesigwa amesema kwamba ni jambo kubwa klabu inapofikisha miaka 80 kuendelea kuwemo kwenye mfumo wa soka kwani vilabu vingi vimeshindwa kuwemo kwenye mfumo huo kama ilivyo kwa Simba.

Aidha amewapongeza kwa kusherehekea vyema siku yao ya Simba day kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya timu ya AFC Leoperd kutoka nchini Kenya
Hata hivyo Mwesigwa amevitaka vilabu vingine navyo kuiga mazuri yanayofanywa na klabu ya Simba hasa katika swala zima ambalo linaleta chachu ya maendeleo kwenye mpira wa miguu.

No comments