YANGA YAWA YA KWANZA KUKAMILISHA USAJILI WAKE,TFF YASEMA ADHABU YA DOLA 500 INAWEZA KUPUNGUA


Timu ya soka ya Yanga imekua timu ya kwanza kukamilisha zoezi la usajili wa wachezaji kwa njia ya TMS kwa timu ambazo usajili wao ulikua na dosari huku nyingine ikiwemo Yanga kushindwa kuwasilisha kwa wakati husika juu ya tarehe ya mwisho ya usajili.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,msemaji wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mara baada ya shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA kufungua dirisha la usajili wa wachezaji hapa nchini kwa masaa 48 baada ya maombi ya vilabu hivyo kuwasilisha utetezi wao Yanga imetumia fursa hiyo kuwasilisha mapema na zoezi lao limeshakamilka

Lucas amesema kwamba mbali na Yanga pia TFF inaendelea kupokea usajili wa timu nyingine ili kufanikisha mchakato huo ambao umekua ukizungumzwa mara kwa mara na wadau wa soka kwa wiki hii

Aidha shirikisho hilo la mpira wa miguu hapa nchini limeshindwa kuweka bayana adhabu ambayo vilabu hivyo vitakumbana navyo baada ya kusema kwamba wanasubiri ufafanuzi kutoka FIFA

Awali shirikisho hilo lilisema kwamba klabu ya ligi kuu inapaswa kulipa dola 500 kwa mchezaji ambae usajili wake haujakamilika huku klabu za daraja la kwanza zikitakiwa kulipa dola 250.

"Hayo ngoja tuyaache juu ya adhabu hizo ingawa yapo kwenye kanuni kwani hata mahakamani akimu anaweza kukupungizia adhabu ya kosa ulilotenda"alisema Lucas.

Hata hivyo Lucas amevitaka vilabu vya Tanzania kufuata taratibu za TFF ili kuondoa migongano isio na tija katika maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

No comments