YANGA YATAKIWA KULIPA DOLA 500 KWA KILA MCHEZJI


Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limesema kwamba, FIFA bado hawajatoa majibu juu ya swala la timu ambazo zimeshindwa kukamilisha usajili wa wachezaji kwa njia ya TMS licha ya timu hizo zote kukamilisha utetezi wao

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kua kwa sasa kuna matumaini kwa timu hizo kufunguliwa dirisha la usajili lakini kilicho kila timu itawajibika kulipa faini kwa mujibu wa taarifa ya awali ambayo shirikisho hilo wamezipata

Amesema kwamba kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA ni kwamba klabu ya ligi kuu inatakiwa kulipa dola 500 kwa kila mchezaji huku timu za daraja la kwanza na la pili zinatakiwa kulipa dola 250.

No comments