FIFA YAIFUNGULIA YANGA TMS ILI IKAMILISHE ZOEZI LA USAJILI


Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limefungua mtandao wa usajili wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa lengo la kuzipa klabu za Tanzania kukamilisha zoezi la usajili kwa timu ambazo usajili wao umekua na kasoro ikiwemo Yanga na Coastal Union ambazo timu hizo hazijawasilisha usajili wa wachezaji wote.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF,inasema kwamba FIFA wametoa muda wa masaa 48 kwa timu hizo kukamilisha zoezi hilo hivyo dirisha la usajili litakua wazi hadi siku ya jumapili saa sita usiku.

Hata hivyo shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba kwa taarifa zaidi kwa klabu hizo zinapaswa ziwasiliane na meneja wa  wa TMS Jonas Kiwia.

No comments