TFF WAZITAKA YANGA NA COASTAL UNION KUWASILISHA UTETEZI WAO KWA KUSHINDWA KUKAMILISHA USAJILI WAO


Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limezitaka klabu za Yanga na Coastal Union kuwasilisha utetezi wao katika shirikisho hilo juu ya kushindwa kuwasilisha majina ya usajili wa wachezaji watakaowatumia kwenye msimu ujao wa ligi kuu na ligi daraja la kwanza kwa mfumo wa TMS

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba hadi dirisha la usajili lilipofungwa ni klabu mbili pekee za Yanga na Coastal Union ndizo zimeshindwa kuwasilisha majina ya wachezaji

Amesema kwamba kwa sasa TFF inasubiri kupata utetezi wa vilabu hivyo ili kujalibu kuliomba shirikisho la mpira wa miguu FIFA kuziruhusu timu hizo zikamilishe zoezi hilo endapo kama sababu zao zitakua na mashiko

Lucas amedai kua ameshangwazwa na klabu ya Yanga kushindwa kukamilisha zoezi hilo ilihali wapo kalibo na ofsi za TFF,huku akisema kwamba viongozi wa klabu hiyo hawakuwa makini kwenye zoezi hilo kwani walishindwa kuhudhuria hata semina ya ufanikishaji wa jambo hilo

Hata hivyo amesema kwamba endapo sababu zao ambazo zitatolewa hazitakua na msingi basi timu hizo zitakumbana na adhabu ya kushushwa daraja hadi daraja la tatu ambapo huko hakuna mfumo wa usajili kwa njia ya TMS
Katika hatua nyingine Lucas amesema kwamba ingawa viongozi wa Yanga wanasema kua wamewasilsha majina katika shirikisho hilo lkn taarifa hizo si za kweli

Lucasi amesema usajili ambao umewasilishwa na Yanga ni wa CAF ambao ni kwa ajili ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika lkn huu wa sasa ambao unatambulika na FIFA klabu hiyo haikuwasilisha

Nao uongozi wa klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga umesema kwamba kwa upande wao zoezi la usajili wa wachezaji ambao watawatumia katika msimu ujao kwenye ligi daraja la kwanza wamelikamilisha mapema

Msemaji wa timu hiyo,Osca Asenga amesema kwamba wao zoezi hilo la usajili wamelifanya kwa weledi tena kwa mfumo unaotakiwa hivyo kama TFF,wanadai hawajapata majina basi yawezekana na matatizo ya kimtandao.

No comments