RAGE AZIPONGEZA SIMBA NA YANGA KUKUBALI MFUMO MPYA WA UENDESHAJI WA SOKA



Aliyekua mwenyekiti wa klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam,Ismail Aden Rage amezipongeza Simba na Yanga baada ya wanachama wake kukubali kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko katika uendeshaji wa mpira

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,Rage amesema kwamba jambo hilo ni zuri na alishawai kulifanya wakati wa uongozi wake ispokuwa kulikua hakuna mwitikio mzuri kama huu wa sasa

Amesema kwamba mbali na wanachama wa klabu hizo kuridhia lkn ni vyema viongozi husika wakawa makini na mikataba watakayoingia na wahusika wanaohitaji kuwekeza kwenye timu hizo.

Hata hivyo amesema kwamba ni vyema mfumo huo ukatambulika kama mapinduzi wala sio mabadiliko kama inavyozungumzwa na wadau wa soka kwa sasa.

No comments