COASTAL UNION WAKAMILISHA UTETEZI WAO KWA TFF


Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya mkoani Tanga,umesema kwamba  tayari wameshawasilisha utetezi wao kwenye shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF baada ya kushindwa kukamilisha usajili wa wachezaji ndani ya siku husika

Kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo,Salum Bawazil amesema kwamba kwa sasa wasubiri maamuzi ya TFF,juu ya jambo hilo kwani haikuwa dahimra yao kushindwa kukamilisha swala hilo kwa wakati wa mwafaka

Amesema kwamba sababu kubwa ambayo ilikua tatizo ni swala zima la mtandao kusumbua katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji


Katika hatua nyingine Bawaziri amesema kwamba wachezaji ambao wamewasajili msimu huu anaamini watakua msada mkubwa kwa timu kwani ni wachezaji wazuri ambao wanacheza soka kwenye mazingira yeyote

Amesema kwamba nia yao ni kuona msimu ujao wanarejea katika ligi kuu ya Tanzania bara hivyo amewataka wanachama na mashabiki wa klabu kwa sasa kuungana pamojana na kuondoa migogoro isio na tija

No comments