YANGA KUPAA ALHAMISI KUWAFUATA USM ALGERS,UONGOZI WAELEZA MCHAKATO WA USAJILI

Na,Said Ally
Kikosi cha  mabingwa wa kihstoria  wa ligi kuu ya vodacom Tanzania Yanga sc alhamisi hii kitasafiri kuelekea  Algeria  tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi  ya kombe la  shirikisho dhidi ya wenyeji USM Algers.

Mjumbe wa kamati ya utendaji ndani ya klabu ya Yanga na katibu wa kamati ya mashindano,Samuel Lukumay alisema kuwa matayarisho ya mchezo huo yanakwenda  vizuri na dhamira yao ni kuona timu inaibuka na matokeo mazuri kwenye pambano hilo  ili kutengeneza mazingira  salama  kwenye kundi.

Lukumay alisema kwamba kwa sasa uongozi unaendelea na taratibu nyingine ikiwemo swala la vibali kwa kocha mkuu wa timu hiyo  Zahera Mwinyi pamoja na kufanikisha mchakato wa usajili kwa wachezaji ambao watawaongeza katika hatua hiyo ya makundi.

Alisema kwamba nia yao ni kusajili kwani wana nafasi tatu za kuongeza wachezaji kwa ajili ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika,hivyo mchakato huo wanataraji kuufanya kwa haraka zaidi.

Hata hivyo alishindwa kuweka bayana juu wachezaji hao watakaosajiliwa kama wanatoka wapi na wanamudu kucheza nafasi ipi uwanjani akidai kuwa hilo ni jambo bado lipo mikononi mwa uongozi.

No comments