AJIBU; AWATOA HOFU WANA YANGA
MSHABULIJI nyota wa Yanga Sc, Ibrahim Ajib amesema hana sababu yoyote ya kugoma kuichezea timu yake kama inavyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii.
Ajib amesema kuwa hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuamua kubakia nyumbani kuipigania afya ya mke wake alikuwa tayari kujifungua baada ya miezi 9 ya ujauzito ulikuwa na matatizo mengi kiafya.
"Kuna wakati nilikuwa na hofu kubwa,juu ya maisha ya mke wangu, uja uzito wake toka awali ulikuwa na matatizo mengi, nashukuru Mungu ametujaalia kupata mtoto wa kike,hilo ni jambo jema kwetu kama familia,ndugu na jamaa kwa ujumla"alisema Ajibu.
Akiendelea zaidi Ajib aliweka wazi kusikitishwa na maneno makali anayotumiwa na mashabiki kupitia jumbe za simu wakimlaumu kwa kugoma kwenda kuichezea timu yake kwenye mchezo wa kombe la shirikisho.
"Sina sababu ya kugoma,kucheza mpira ndiyo kazi yangu, hofu kubwa niliyokuwa nayo juu ya afya ya mke wangu kutokana na matatizo ya ujauzito aliokuwa nao hata kama ningeenda nadhani nisingeweza kucheza vizuri, kati yetu hakuna asiyejuwa juu ya matatizo yanayowakuta mama zetu"
Chanzo,Mtandao wa klabu ya Yanga.

Post a Comment