SIMBA WAITISHA MKUTANO WA DHARURA

Uongozi wa klabu ya Simba umeitisha mkutano wa mabadiliko ya katiba utakaofanyika siku ya jumapili ya 20/5/2018.

Kwa mujibu wa taarifa  kutoka katika uongozi wa klabu hiyo,mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo maeneo ya Ocean Road jijini Dar es salaam.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza mishale ya saa tatu asubuhi na siku chache zijazo ajenda na nyaraka  nyingine kama inavyoelekeza katiba ya klabu hiyo ibara ya 22 kifungu namba 4 zitawekwa hadharani.

No comments