LICHA YA KUFUNGWA NA AZAM FC MTIBWA SUGAR WASALIA NAFASI YA SITA

Mabingwa wa ligi kuu bara mara mbili Mtibwa Sugar Sc Jumamosi walicheza mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Azam kutoka jijini Dar es salaam.
Mtibwa Sugar Sc walipoteza mchezo huo kwa goli moja kwa bila, mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini Azam fc waliweza kupata goli kupitia kwa Shaban Idd Chilunda 39′, goli hilo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kufanya mchezo umalizike kwa Mtibwa kupoteza kwa goli 1.
Baada ya matokeo hayo Mtibwa Sugar bado inaendelea kukalia nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi kuu bara ikiwa imefanikiwa kukusanya pointi 33 katika michezo 25.

No comments