TIMU YA MSUVA KUSAJILI MCHEZAJI WA YANGA

Na Said Ally
Mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga,Hussein Nyika amesema kwamba kuna uwezekano mkubwa mchezaji wa timu ya Yanga kusajiliwa na klabu ya Difaa Hassan El Jadidi ya nchini Morocco.

Nyika ameiambia MWANDIKE BLOG kuwa baada ya klabu hiyo kumsajili mchezaji Simon Msuva iliahidi kuendelea kusajili mchezaji kutoka Yanga kwa yule atakaebainika kuwa na kiwango kizuri.

Alisema kwamba kupitia mchezo wa kesho dhidi ya USM Alger kuna nafasi kubwa ya wachezaji wa Yanga kuonekana na viongozi wa Difaa Hassan El Jadidi kwani viongozi hao wapo nchini Algeria na wamewataarifu kuwa watautazama mchezo huo.

Yanga hapo kesho inataraji kushuka dimbani kumenyana na USM Alger katika mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika,mchezo utakaopigwa nchini Algeria.

No comments