MTIBWA SUKARI KUCHEZA UGENINI NA WANALIZOMBE WA SONGEA

Wafalme wa soka kutoka mji kasoro bahari Mtibwa Sugar Sc wanataraji kusafiri kuelekea mkoani Ruvuma kucheza mchezo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League) dhidi ya Maji maji Fc.
Mchezo huo wa Vodacom Premier League unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni siku ya Jumapili katika uwanja wa wa Majimaji Songea.
Mtibwa Sugar imefanikiwa kukusanya pointi 33 na inashikilia nafasi ya 6  katika msimamo wa ligi kuu bara huku Maji maji ikishikilia nafasi ya 14 ikiwa imefanikiwa kukusanya poniti 23 katika msimamo wa ligi kuu bara (Vodacom Premier League).
Takwimu zinaonesha Mtibwa Sugar imekuwa mbabe wa Maji maji katika michezo ya ligi kuu bara (Vodacom Premier League) kwa takribani miaka 8 Mtibwa Sugar Sc imeendelea kuwanyanyasa Majimaji.
Katika michezo 7 ya mwisho timu hizi zilipokutana Mtibwa Sugar imefanikiwa kushinda michezo 5 huku Majimaji wao wakifanikiwa kushinda mchezo 1 na kutoa sare 1, katika michezo hiyo 7 Mtibwa Sugar wamefanikiwa kufunga magoli 9 huku Majimaji wao wakifunga magoli 5.
Katika michezo hiyo 7 waliyokutana katika ligi kuu bara (Vodacom Premier League) michezo 3 imechezwa katika uwanja wa Majimaji na katika michezo hiyo Mtibwa Sugar imeshinda michezo 2 na kupoteza 1.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili ya tarahe 06.05.2018 majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Maji maji Songea, Ruvuma.

No comments