MWAKYEMBE AWAPA TANO SERENGETI BOYS

Na,Said Ally
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema kwamba watanzania wote pamoja na serikali wameupokea kwa furaha kubwa ushindi walioupata timu ya vijana ya Serengeti Boys katika michuano ya CECAFA iliyofanyika nchini Burundi.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari katika mapokezi ya vijana hao ambao wametwaa ubingwa wa CECAFA kwa vijana walio na umri chini ya miaka 17,Mwakyembe alisema kwamba kwa sasa wameanza kuona makombe kwa mara ya kwanza katika nchi yetu baada ya ukame wa muda mrefu.
Mwakyembe alisema kwamba serikali kwa kushirikiana na TFF wamedhamiria kuwekeza katika timu za vijana hasa Serengeti Boys ambayo mwakani itashiriki michuano ya fainali za vijana kwa Afrika ambapo Tanzania itakuwa mwanyeji.

Serengeti Boys ilifanikiwa kubeba taji hilo baada ya kuifunga Somali kwa jumla ya bao 2-0 katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya vijana iliyofanyika nchini Burundi.

No comments