MASHABIKI WA YANGA WAMJIA JUU GEORGE LWANDAMINA

Baadhi ya mashabiki wa Yanga wamesema kwamba kocha mkuu wa klabu hiyo George Lwandamina hastahili kuwepo katika klabu hiyo kwa kuwa hana uwezo wa kuiongoza vyema timu hiyo kwenye mechi mbalimbali.
Mashabiki hao wameyasema hayo baada ya mehi ya jana kuisha kwa timu hizo kufungana bao 1-1 na Zanaco ya Zambia katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika.

Wakiongea na MWANDIKE.BLOGSPOT kwa nyakati tofauti wamedai kuwa tangu aichukue timu hajaleta mabadiliko yeyote mazuri ambayo yangeweza kuisaidia timu zaidi ya kushuka kwa vingo kwa wachezaji.

"Timu haijulikani inacheza mfumo gani,angalia sub anazofanya eti anamtoa Thabani Kamusoko anamuingiza Juma Mahadhi wakati sehemu ya kiungo haichezi vizuri,unampanga Yondani namba sita unategemea nini,nakwambia wewe ngojea ndugu mwandishi siku utasiki Dida kapangwa namba tatu"alisema shabiki.
Hata hivyo baadhi yao wakaafikia jukumu la kusema ni bora uongozi uachane na kocha huyo ili wamrejeshe Hans van Der Pluijm ambae kwao wameona amekuwa na mafanikio makubwa kwa kuiongoza vyema timu hiyo na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

No comments