HANS VAN DER PLUIJM ATUA SINGIDA UNITED

Aliyewai kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga na pia akiwa mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo kabla ya kutupiwa vilago vyake na uongozi wa klabu hiyo, Hans van Der Pluijm yuko mbioni kujiunga na klabu ya Singida United ambayo imepanda daraja msimu huu.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vinadai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kocha huyo mwenye historia nzuri na klabu ya Yanga kusaini kandarasi ya kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo ya Singida United.


Singida United ni miongoni mwa timu inayosimamiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ambae mara nyingi amekuwa akimuhusudu kocha Hans kutokana na ufundishaji wake na mafanikio aliyoyapata katika klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani.


Hata hivyo klabu hiyo ya Singida United imeshaanza taratibu za usajili wa wachezaji wakiwemo wachezaji kutoka nje ya nchi huku Hans akionekana na moja ya wachezaji hao waliosajiliwa na Singida United.

No comments