YANGA KUWAVAA ZANACO MISHALE YA SAA 10:00 JIONI

Mchezo wa marudiano wa hatua ya 32 bora ya ligi ya mabingwa barani Afrika katika ya Yanga na Zanaco unataraji kupigwa kuanzia mishale ya saa 10:00 jioni kwa saa za hapa nyumbani,mchezo unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa wa Mashujaa,Lusaka nchini Zambia.


Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali ni kwamba hakuna kituo chochote cha TV cha hapa nyumbani ambacho kitaonesha mechi hiyo itayoamua mshindi atakaefuzu katika hatua ya makundi ya klabu barani Afrika.


Yanga katika mchezo wa hii leo wanahitaji ushindi wowote ama kupata sale inayoanzia mabao 2-2 ili ifuzu katika hatua hiyo,ambapo kwa mujibu wa winga wa timu hiyo Saimon Msuva amesema kwamba wachezaji wote wapo katika hali nzuri na wataingia kwenye pambano hilo kwa nguvu kuhakikisha wanaibuka kwenye pambano hilo.

No comments