EL-MAAMRY AKEMEA UPANGAJI WA MATOKEO KWA TIMU ZA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

Mjumbe wa kudumu wa CAF,Said El-Maamry amezitaka timu za Tanzania bara na Zanzibar kuonyesha ushindani mkubwa wa kimchezo pale wanapokutana katika ushiriki wa michezo mbalimbali ili kuondoa hofu iliyojengeka kwa baadhi ya nchi kwamba huenda timu hizo zitaachiana pale zinapokutana hasa mmoja anapohitaji nafasi ya kushinda.


El-Maamry aliyasema hayo baada ya Zanzibar kupata uwanachama kamili wa CAF ambapo kwa muda mrefu viongozi mbalimbali kutokana Tanzania bara na Zanzibar walikuwa wanalipigania swala hilo.


Alisema kuwa ni jambo la faraja kuona Zanzibar inapata uwanachama kamili wa CAF kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakipigania swala hilo lakini wamekuwa wakigonga mwamba,hii inatokana na baadhi ya nchi kutohitaji swala hilo.


Aidha amedai kuwa kwa sasa kilichopo ni kuona Zanzibar inafanikiwa kupata uwanachama kamili wa FIFA kwani sifa na sababu za kuwa mwanachama wa shirikisho hilo zipo hasa baada ya kukamilika kwa uwanachama wa CAF.



No comments