Baada ya uongozi wa klabu ya Singida United kumpa kandarasi ya miaka miwili kocha Hans van Der Pluijm kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo inayotaraji kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao,leo hii uongozi huo umeweka bayana juu ya mipango yao ya usajili.
Katibu mkuu wa Singida United,Abdulrahamani Salum Sima amiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kuwa klabu hiyo imelenga kusajili wachezaji watano kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukiboresha kikosi cha timu hiyo.
Sima alisema jukumu hilo kwa sasa wameliacha kwa kocha mkuu Hans pamoja na msaidizi wake Fredlick Minziro ambao watakuwa na kazi kubwa ya kulisimamia vyema benchi hilo la ufundi kwa kusajili wachezaji mbalimba wa nje ya nchi na ndani.
Alisema kuwa uongozi umepanga kusajili wachezaji watano wa kimataifa lakini kunaweza kuwepo kwa mabadiliko juu ya wachezaji hao endapo benchi la ufundi la timu hiyo litakuwa na mapendekezo mengine juu ya usajili.
Post a Comment