SINGIDA UNITED YAMTAMBULISHA RASMI KOCHA HANS

Uongozi wa timu ya Singida United inayotaraji kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao umeweka bayana juu ya taarifa za kocha Hans van Der Pluijm kujiunga na klabu hiyo iliyopanda daraja msiu huu.


Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari kupitia kwa katibu mkuu wa klabu hiyo Abdulrahaman Salum Sima imesema kwamba klabu hiyo imeingia makubaliano na kocha Hans kwa kandarasi ya miaka miwili kuwa kocha mkuu atakaerithi mikoba ya Fredlick Minziro aliyeipandisha timu kutoka ligi daraja la kwanza.


Mbali na Hans klabu hiyo pia imeshakamilisha usajili  kiungo wa kimataifa Tafadazwa Kutinyu kutoka timu ya Chicken Inn inayoshiriki ligi kuu nchini Zimbabwe.


Hata hivyo uongozi huo umesema kwamba Kocha Hans van Pluijm atakabidhiwa fungu kubwa la fedha za usajili kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji wa timu hiyo ambao nia yao ni kuona msimu ujao Singida United inakuwa tishio katika ushiriki wa michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments