YANGA KWENDA ZAMBIA NA WACHEZAJI 20


Uongozi wa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu  bingwa barani Afrika Yanga SC umeweka bayana juu ya  taarifa ya safari yao hapo kesho kuelekea Zambia katika mechi ya marudiano dhidi ya Zanaco FC.


Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka kesho jioni majira ya saa 11:15 kwa ndege ya shirika la Kenya Airways.


Wachezaji wanaondoka ni Makipa; Deogratius Munishi na Ali Mustafa . Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.


Nafasi ya viungo ni; Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke, Justine Zulu,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva na Geofrey Mwashuiya. Upande wa washambuliaji ni Obrey Chirwa na Emanuel Martin.


Wachezaji wafuatao wataukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali zikiwemo majeruhi ; Malimi Busungu, Mateo Antony , Pato Ngonyani , Amisi Tambwe , Yusufu Mhilu na Donald Ngoma.

No comments