YANGA KUTUMIA KENYA AIRWAYS KUWAFUATA ZANACO

Msafara wa klabu ya soka ya Yanga mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara , utaondoka alhamisi nchini kuelekea nchini Zambia katika mechi ya marudiano na Zanaco FC kwa Ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways.


Msafara wa Yanga SC utakuwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi . Yanga inaelekea Zambia katika mechi ya marudiano klabu bingwa Afrika baada ya mechi ya awali jumamosi kutoka sare ya 1-1 na Zanaco FC uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.


Timu inaendelea vyema na mazoezi kuelekea mchezo huo  wa marudiano utakaochezwa siku ya Jumamosi.


Wanachama na wana Yanga Sc kama ilivyo kawaida yetu twende kwa wingi tukawape nguvu vijana wetu kwenye mchezo huo.

Katika mchezo huo Yanga inahitajika kushinda kwa ushindi wowote ili ifanikiwe kufuzu katika hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

No comments