TRA YAZIFUNGA OFISI ZA TFF

Mamlaka ya mapatao Tanzania (TRA) imezifungia ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF na kuamrisha wafanya kazi kuacha kila kitu ndani ya ofsi hizo zilizopo Karume jijini Dar es salaam kutokana na shirikisho hilo kudaiwa deni la kodi linalojumuisha kodi za mapato na kodi za ajira.


Afisa Habari wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo amesema kwamba wameamua kuchukua jukumu hilo kutokana na TFF kutolipa madeni hayo kwa muda mrefu hadi kufikia sasa.


Amesema kwamba hatua hii ambayo wameichukua ya kuzifunga ofisi hizo ni ya mwisho baada ya kuonekana hatua zote za kufanikisha kupata kodi hizo zimeshindikana.


Hata hivyo ameendelea kusema kuwa TRA hawatazifungulia ofisi hizo pasipo shirikisho hilo ambalo lina hodhi mpira wa miguu hapa nchini kutolipa madeni hayo ya muda mrefu.


No comments