WATAKAOIKASHIFU SERIKALI KWENYE MECHI YA YANGA NA NGAYA KUCHUKULIWA HATUA KALI

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limesema kwamba litawatia nguvuni mashabiki wataoikashifu Serikali ama uongozi wa shirikisho hilo kwa kuingia na mabango uwanjani yenye ujumbe tofauti hapo kesho katika mchezo wa kimataifa wa klabu bingwa barani Afrika kati ya Yanga ambao ndio wenyeji dhid ya Ngaya ya Comoro.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari,afisa habari wa shirikisho hilo Alfred Lucas alisema kwamba TFF imebaini kutokea kwa jambo hilo hivyo ni vyema wakatoa tahadhari mapema kabla ya mashabiki kutovunja sheria ya nchi.

No comments